UTANGULIZI:

Mpango wa Taifa wa kudhibiti na kuratibu silaha ndogo nchini Tanzania, ni mpango wa miaka mitano wa uendelezaji wa miradi inayohusisha sekta zote, wenye malengo ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza uzagaaji haramu wa silaha ndogo. jitihada za kwanza za mpango huu, na dunia kwa ujumla zimeanzishwa kwa uanzishwaji na uendelezwaji wa mipango ya utafiti, kuhusisha jitihada za pamoja za kitaifa na kimataifa na jamii kwa ujumla, katika kupambana na tatizo hili.jitihada hizi za uendelezaji na utekelezaji wa mpango huu waTaifa zimethibitisha kuwa zitakuwa bora na zenye mafanikio. Utekelezaji huu umeanza tarehe I februari, 2002.

KWA NINI TANZANIA:

Ukanda wa nchi za Maziwa Makuu ya Afrika zimekuwa ni nchi zinazosumbuliwa na uzagaaji wa silaha ndogo, pamoja na nchi za Kati, Kusini na Mashariki. Kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita, kutokana na mapambano ya kudai uhuru na ukombozi wa Mwafrika, eneo hili limeathirika sana.
Eneo hili limeathirika kutokana na vita baridi vilivyokuwa vinaendeshwa, na eneo lilionekana kama uwanja wa vita. Kutokana na vita baridi hivyo, na mapambano ya kudai uhuru, kumepelekea kuwepo kwa wanajeshi wengi wenye ujuzi mdogo ambao waliachwa kutokana na migogoro hiyo. Kuwepo kwa silaha ndogo nyingi pamoja na risasi kumeliathiri sana eneo hili.
Vyanzo vya upatikanaji wa silaha ndogo katika eneo hili ni vya zamani na vile vile vipya. Si kwamba silaha zote zilizo katika mzunguko zimesababishwa na sababu hizo. Kutokana na Kuwepo kwa mchanganyiko wa vyanzo vya kuzagaa silaha haramu, katika eneo hili, na katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla, mpango madhubuti wa kutokomeza uzagaaji huu unahitajika sana. Zaidi ya hapo, msisitizo unahitajika kwa serikali ya Tanzania kufanya jitihada za kipekee katika kupambana na uhalifu, ugaidi na silaha haramu katika nchi za Kusini, Mashariki na Afrika ya Kati.

Sababu zinazoipa umuhimu nchi ya Tanzania. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishiriki kwa dhati katika jitihada zote za kitaifa na kimataifa katika kutunga sheria za kupambana na uzagaaji wa silaha, na biashara haramu ya silaha. Kwa kujihusisha kwake huko, si to kwamba imetoa mchango thabiti, bali pia imethibitisha kwamba makubaliano yanalenga kwenye mahitaji yaliyoazimiwa.
Mpango wa utekelezaji wa Itifaki yaVienna,Azimio la OAU la BAMAKO, Itifaki ya SADC ihusuyo silaha na risasi, Azimio la Nairobi, Itifaki ya Afrika Mashariki ya Silaha zinazotoa miongozo ya kitaifa na kimataifa na zote zipo katika utekelezaji.
Makubaliano yote haya yanatoa misingi imara ya kisiasa ambayo kwayo yatasaidia kukabiliana na uzagaaji wa silaha ndogo na yametoa mwongozo mzuri wa uanzishwaji wa mpango wa taifa waTanzania.

MAAMUZIYA KITAIFA:

Kwa kuwa maamuzi haya ya kitaifa na kimataifa yametoa msingi imara wa kisiasa, ni ngazi ya kitaifa sasa yenye jukumu la utekelezaji wa mipango hiyo kwa vitendo. Kwa kujua haja ya haraka ya utekelezaji wa mpango huo, serikali W Tanzania imeanzisha vyombo vitakavyosimamia utekelezaji wa makubaliano au mipango hiyo.Vyombo vikuu vitatu vilianzishwa mwaka 2001 ambavyo ni: Kwa kuanzisha vyombo hivi, Serikali ya Tanzania ilihakikisha kuwa washika dau wote wanashirikishwa/wanahusishwa.Vile vile Mamlaka za mikoa na mitaa, wakala wa Serikali na jamii ya Watanzania kwa ujumla ni sehemu muhimu sana kwa vyombo vyote hivyo vitatu. Baada ya vyombo hivyo vya Serikali kuanzishwa hatua iliyofuata ya kuendeleza mpango waTaifa ni kuhakiki hali ya silaha ndogo NchiniTanzania. Kamati yaTaifa ilianzisha mpango thabiti wa kuhakiki hali hiyo NchiniTanzania. Malengo ya zoezi hilo yalikuwa ni kuona hali, na kiasi cha uzagaaji wa silaha, kulinganishwa na mahitaji na upatikanaji, uwezo uliopo, na nyenzo zilizopo za kulielezea tatizo, mtazamo na uzoefu wa Watanzania kuhusiana na uzagaaji wa silaha ndogo.Taarifa hizi kwa mfano zilipatikana baada ya watu kuhojiwa, kufanya makongamano, na tafiti mbalimbali zilizofanywa kushirikiana na vyama mbalimbali vya Kitaifa na Kimataifa visivyo vya kiserikali. Kwa upande mwingine Serikali ilifanya uhakiki wake kuona uwezo wake kisheria wa kushindwa kuzuia kupenya kwa silaha haramu kupitia maeneo muhimu yaliyo nchini. Uhusiano na mawasiliano kati ya sekta zote za kijamii zilizo za kiserikali na sizizo za kiserikali vilikuwa ni vitu vya msingi katika zoezi hili.

Matokeo ya zoezi hili la Kitaifa yaliipatia Serikali ya Tanzania taarifa muhimu ambayo ingeweza kutumika katika kurekebisha mfumo kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo waTaifa, na ikibidi kufanya marekebisho kabisa ya mfumo mzima, au kuanzisha mfumo mpya. Usanifu wa utekelezaji wa mpango huu wa Taifa uliopatikana Novemba 2001 ni kama ifuatavyo: Mbali ya vyombo hivi, Kamati ya Taifa ya kuongeza uwezo wa kifedha imeanzishwa ili kuhakikisha kwamba miradi iliyoanzishwa inaimarika kwa kutumia uwezo uliopo na kuongeza fungu la fedha lililopo kwa lengo la kuendeleza, katika kipindi cha miaka mitano, miradi imara na inayojitegemea.

MPANGO WATAIFA WA UTEKELEZAJI:

Taratibu zilizoelezewa hapo juu ni vyombo ambavyo utekelezaji wa miradi - madhumuni ya mpango waTaifa, zinategemewa kwa ajili ya utekelezaji. Mpango waTaifa wa utekelezaji unahusisha nyanja mbalimbali na miradi ambayo inatekelezwa kwa. pamoja kati ya Serikali na mawakala wa jumuia za kijamii.
Ratiba ya miradi hiyo imeandaliwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo utafanywa kwa usahihi katika kipindi chote cha miaka mitano.
Uanzishwaji wa miradi, kwa ajili ya mpango wa Taifa, umefanywa kwa kuhusisha maeneo yote, na uhakiki wa sekta zote nchini Tanzania, mwishoni mwa mwaka 2001.
Kila sehemu au mradi una wakala wake na vyama visivyo vya Kiserikali vya Tanzania vitakuwa na mwakilishi wake atakayehusika moja kwa moja akisaidiwa na wajumbe wa kamati ya Taifa, mawakala wa Serikali, na vyombo vya kijamii. Kila mradi utafanywa kwa hatua, zilizothabiti, ambazo zimeandaliwa ili zilingane na uwezo wa kifedha uliotengwa.
Zaidi ya miradi 100 midogo midogo imethibitishwa kwa ajili ya utekelezaji katika hatua mbalimbali. Kila eneo/nyanja linalohusu silaha ndogo nchini linapewa kipaumbele. Hivyo kuna miradi inayoangalia au inayodhibiti hazina ya silaha, na kuimarisha udhibiti wa mipaka, na kuna He inayojihusisha na kupunguza hali ya utegemezi, kwa kutoa elimu kwa jamii na kuanzisha shughuli za kiuchumi. Vile vile, si miradi yote yenye sifa na muonekano wa kitaifa. Miradi mingi imelenga katika kuimarisha mahusianao kati ya Tanzania na majirani zake na mingine ipo kwa ajili ya kuboresha uwezo wa sekratariati wa nchi za Kusini na Mashariki ya Afrika kwa kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na tatizo la biashara haramu ya silaha.
Hivyo, mpango huu wa Taifa wa Tanzania unajumuisha mfumo muunganifu unaohakikisha ubora wa udhibiti wa miradi midogo. Miradi hii midogo imetengwa katika sehemu ndogo ndogo. Sehemu kuu sita za mpango wa Taifa zinaweza kuelezwa kwa. ufupi kufuatana na mambo yafuatavyo: Miradi yote midogo, inafadhiliwa na mpango wa muda mrefu, ambao unajishuhulisha na uanzishwaji wa nguvu za pamoja za kulishuhulikja tatizo la silaha ndogo, uanzishaji wa nyenzo ambazo zitatoa ufafanuzi wa jinsi ya kulitatua tatizo husika, na utekelezaji wa mpango wa kuratibu na kudhibiti silaha, ndani na nje ya nchi. Kwa kuwa na taratibu hizi, Watanzania wanaweza kuchukua hatua maridhawa za kuzuia, kuondoa, na kutokomeza kabisa tatizo la silaha ndogo kwa njia iliyo bora.
Moja ya vigezo ambavyo, mpango huu wa Taifa unautumia ni kwa kufanya kazi iliyo sahihi. Matokeo yake ni upatikanaji wa gharama, zilizopatikana katika hatua mbili.
Bajeti ya kwanza ya mradi imepatikana kufuatana na uwezo uliokuwepo kuweza kufadhili mradi, bila kutegemea ufadhili wa nje. Katika hatua ya pili, uhakiki wa gharama umefanywa ili kujua ni shughuli gani zingehitaji kuombewa fedha ya ziada. Hata hivyo, katika hatua zote, gharama za miradi zimekamilishwa na pesa za Serikali. Kwa misaada toka nje ya nchi, Serikali yaTanzania iliomba kutoka Serikali ya Uingereza na Ubalozi wa jumuia ya Ulaya.
Serikali ya Uingereza imetoa ongezo la fedha za kuanzia miradi ambao utekelezaji wake umeanza tarehe I Februari 2002.

HITIMISHO - MAENDELEO BAADAYA MAKUBALIANO:

Mpango wa Taifa wa utekelezaji unaonyesha taratibu za kuzuia, kuondoa na kutokomeza uzagaaji wa silaha ndogo ni taratibu ambazo zimepatikana baada ya kuwepo mipango ya pamoja, iliyoonyesha haja ya kushirikisha jamii, ili hali ya amani, usalama na maendeleo iweze kupatikana. Wakati mpango huu wa Taifa unalenga katika kuratibu na kudhibiti silaha ndogo, mafanikio yake si to kwamba yatalenga katika silaha na usalama, lakini pia katika utawala bora wa serikali, demokrasia, uaminifu na maendeleo, kwani msingi wake umeanzishwa na kutekelezwa na Watanzania, na utawanufaisha Watanzania wote kwa ujumla.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Kamanda wa Kitengo cha Kuratibu na Kudhibiti silaha ndogo,
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, S.L.P 9093,
Dar es Salaam. Tanzania,
Simu 255 22 213 2252 au

Mr. Jakkie Potgieter,
Mkurugenzi Safer Africa,
AMAD Appointed Manager
173 Beckett Street,Arcadia
Pretoria 0083, South Africa
Tel: 27-12-344-6700
Fax: 27-12-344-6708
www.saferafrica.org
Email: safe rafrica@saferafrica.co.tz

Centre of Peace and Economic Development - CEPEDE
1st Floor ZahraTower (MZ02)
Corner of Zanaki and Indira Ghandi Street
Dar es Salaam
Tel: + 255 2 213 6391
Fax: + 255 2 21 213 6393
Email: cepede@africaonline.co.tz



about us | events | programmes | publications | contact us

Copyright © 2006 SaferAfrica